WAUMINI MSATA, MBOGA WANUFAIKA NA MRADI WA UWEZESHAJI WA KIUCHUMI.

 WAUMINI MSATA, MBOGA WANUFAIKA NA MRADI WA UWEZESHAJI WA KIUCHUMI.

Mnamo Oktoba 11, 2022 Afisa Mtendaji Mkuu wa Bilal Muslim Mission of Tanzania (BMMT) ndugu Hafidh Mansour alifanya ziara katika vituo vya Mboga na Msata ambapo pamoja na mambo mengine alifanikisha zoezi la utoaji wa fedha takriban shilingi milioni 10 nalaki sita za Tanzania zenye malengo ya kuwawezesha waumini kiuchumi.

Katika ziara hiyo ya siku moja, Afisa Mtendaji Mkuu aliambatana na Afisa Miradi wa BMMT ndugu Muhammad Mbaga ambapo awali aliongoza semina maalumu juu ya usimamizi wa fedha na uendeshaji wa biashara kabla ya kukabidhi fedha hizo.

Jumla ya waumini 33 kutoka kituo cha Mboga na 15 kutoka kituo cha Msata walikabidhiwa pesa hizo ambazo watazitumia kufanya biashara mbalimbali, kilimo na shuguli nyingine za uzalishaji mbali huku wakizirejesha kidogo kidogo bila ya riba ili fedha hizo zitumike kuwawezesha waumini wengine.

Kwa niaba ya waumini, BMMT inatoa shukrani kwa Africa Federation (AFED) kwa kufadhili mradi huu muhimu kwa ajili ya maendeleo ya jamii yetu.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *