Islamic Corresponding Course/Masomo ya Kiislamu

Tunatoa Programu ya Masomo ya Kiislamu mahususi kwa ambaye hakupata fursa ya kupitia kwenye mfumo rasmi wa madrasa au shule inayofundisha masomo ya dini lakini pia kwa yeyote ambaye angependa kujifunza hata kama si muislamu. Programu hii imegawanywa katika madaraja mawili:

Masomo ya Msingi ya Kiislamu

  • Madhumuni: Inatoa mafunzo ya awali ya Kiislamu, ikiwafaa zaidi wale wanaoanza na kutaka kuimarisha uelewa wao juu ya mafundisho ya Uislamu.
  • Yaliyomo: Inajumuisha vitabu vinne muhimu, vinavyoangazia na kutoa utangulizi juu ya nyanja kuu za Uislamu

Masomo ya Juu ya Kiislamu

  • Madhumuni: Inawalenga wale wenye maarifa ya msingi na wenye kutaka kujua zaidi na kuimarisha uelewa wao wa kitaaluma juu ya mafunzo ya Kiislamu.
  • Yaliyomo: Inajumuisha vitabu vinne vinavyoangazia masuala makubwa ya kitaaluma kuhusu Uislamu.

Njia za Kujifunza

  • Masomo ya Kiislamu kwa Njia ya Posta: Katika njia hii, mwanafunzi anatumiwa vifaa vyake vya kujifunza (Vitabu) kwa njia ya Posta na atatumia njia hiyihiyo kutuma mitihani.
  • Masomo ya Kiislamu kwa Njia ya Mtandao: Katika njia hii, mwanafunzi atapata vifaa vyake vya kujifunza (Vitabu) kwa njia mtando mfano kupitia tovuti, baruapepe au namba ya whatsapp na atatumia njia hizo kutuma mitihani.

Chaguo hizi mbili, zinampa mwanafunzi uhuru wa kusoma kwa njia ambayo inaendana na mtindo wake wa maisha.

Aidha, mwanafunzi atasoma kwa kasi yake mwenyewe hadi miezi minne kwa kila daraja. Tunafanya hivi kwa kutambua kuwa, mwanafunzi tunayemlenga ni mtu mzuma (miaka 16+) ambaye huenda atatingwa na shughuli nyingne aisha za kimasomo au kikazi.

Usajili

Kwa maelezo zaidi au kujisajili katika programu, na msaada zaidi tafadhali wasiliana na mratibu wa programu. Tunahakikisha hakuna mtu anayepitwa na neema ya kuujua Uislamu.

MASOMO YA MSINGI YA KIISLAMU

MASOMO YA JUU YA KIISLAMU

Baada ya kujaza fomu ya usajili, itume kwa Mratibu wa Programu kupitia Sanduku la Posta 20033, Dar es Salaam au kupitia baruapepe: bookshop@bilal.or.tz au namba ya simu +255 678 888 795 (Whatsapp)

ZINGATIA: kwa mwanafunzi wa masomo ya juu ya kiislamu, hakikisha unaambatanisha nakala ya cheti cha Masomo ya Msingi ya Kiislamu (PDF)

“Kutafuta elimu ni wajibu kwa kila Muislamu, mwanaume na mwanamke.”

Mtume Muhammad (s.a.w.w)