BMMT YAWAANDAA MUBALIGHAT KUPITIA SEMINA MAALUM YA SIKU TATU
Dar es Salaam, Tanzania – 16 Julai 2026
Taasisi ya Bilal Muslim Mission of Tanzania (BMMT) imeandaa semina maalum ya siku tatu kwa wanawake wanaotekeleza majukumu ya tabligh, maarufu kama Mubalighat. Semina hiyo itafanyika kuanzia tarehe 17 hadi 19 Julai 2026, katika Hawzat Maasoomat, Ubungo–Mabibo, Dar es Salaam.
Semina hiyo inalenga kuwaongezea na kuwaimarisha Mubalighat maarifa, stadi na uwezo wa kutekeleza kwa ufanisi majukumu yao ya kufikisha ujumbe wa dini, kutoa malezi ya kiroho na kuchangia katika maendeleo ya jamii.
Katika semina hiyo, washiriki watapata mafunzo kutoka kwa wakufunzi mahiri na wenye uzoefu katika nyanja mbalimbali. Mafunzo yatajikita katika kuimarisha uwasilishaji wa ujumbe, mbinu za ufundishaji, mawasiliano yenye matokeo, uongozi na namna bora ya kukabiliana na changamoto zinazojitokeza katika shughuli za tabligh.
Kupitia semina hii, BMMT inaendelea kuthibitisha dhamira yake ya kuwajengea uwezo Mubalighat ili waweze kutekeleza majukumu yao kwa weledi, maarifa na ufanisi zaidi katika kuitumikia dini na jamii.
Muhimu: Semina hii ni kwa washiriki walioalikwa pekee.
Download Press pdf
UPSKILL PRESS
