84 WATUNUKIWA VYETI PROGRAMU YA MASOMO YA KIISLAMU KWA NJIA YA POSTA & MTANDAO.

 84 WATUNUKIWA VYETI PROGRAMU YA MASOMO YA KIISLAMU KWA NJIA YA POSTA & MTANDAO.

Wanafunzi 84 walitunukiwa vyeti vya kuhitimu programu ya Masomo ya Kiislamu kwa njia ya Posta na Mtandao.
Hafla ya kutunuku vyeti hivyo ilifanyika mnamo Oktoba 15, 2022 katika Husaynia ya Bilal Temeke na kuhudhuriwa na wageni mbalimbali mgeni rasmi akiwa Mdiru wa Hawzatu Bilal Temeke – Sheikh Muhammad Yusuph.

Mambo mbalimbali yalifanyika wakati wa mahafali hayo ikiwemo kufunguliwa kwa kisomo cha Qur-an, na kufunga kwa dua’a kabla ya swala ya jamaa ya dhuhri na chakula cha pamoja.

Miongoni mwa waliokuwa wazungumzaji wakubwa ni pamoja na mgeni rasmi, Sheikh Muhammad Yusuph na mgeni mwalikwa Sheikh Ramadhan Kwezi ambao wote wamezungummzia umuhimu wa programu hii na kutoa wito wa kuendelezwa kwa manufaa ya jamii.

Katika mwaka huu wa 2022, jumla ya wanafunzi 174 walidahiliwa wakiwemo 165 waliokuwa wanasoma kwa njia ya Posta na wengine 9 wakisoma kwa njia yaMtandao ambapo wanafunzi 84 sawa na asilimia 48.3 wamehitimu na kutunukiwa vyeti.

Programu hii ilianzishwa na muasisi wa Bilal Muslim Mission of Tanzania (BMMT) Allamah Sayyid Saeed Akhtar Rizvi mnamo mwaka 1972 na ilifanya mahafali yake ya kwanza mnamo mwaka 2021.

Programu ya Masomo ya Kiislamu kwa njia ya Posta na Mtandao inaratibiwa na Bilal Muslim Mission of Tanzania (BMMT) na inatolewa bure kabisa kuanzia Usajili, Vitabu, Mitihani na Vyeti ikiwa na malengo ya kuhakikisha kuwa kila mmoja anapata neema ya kuujua Uislam halisi kama ulivyoelekezwa na Mtukufu Mtume Muhammad (s.a.w.w).

kujua zaidi kuhusu programu hii, bofya hapa

Kwa niaba ya wanafunzi na uongozi tunatoa shukrani kwa Africa Federation (AFED) kwa kudhamini progrmau hii.
Tunatoa shukrani zetu za dhati pia kwa Uongozi wa Bilal Comprehensive School (BCS), Uongozi wa Hawzatu Bilal Temeke, na kila mmoja kwa nafasi yake kwa kuifanya shuguli hii kuwa ya mafanikio.

Mratibu wa Programu ya Masomo ya Kiislamu kwa njia ya Posta & Mtandao, Sadah Ally Salum akielezea programu wakati wa hafla ya mahafali ya programu hiyo.
Wanafunzi na wageni waalikwa wakifuatilia mada wakati wa hafla ya mahafali ya Programu ya Masomo ya Kiislamu kwa njia ya Posta na Mtandao.
Wahitimu (jinsia KE) kwenye picha ya pamoja na Mratibu wa Programu (Wanne kutoka kushoto – nyuma) Sadah Ally Salum baada ya hafla ya mahafali.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *