SHEIKH/DKT. MURTAZA ALIDINA AFANYA ZIARA BILAL MAKAO MAKUU.

 SHEIKH/DKT. MURTAZA ALIDINA AFANYA ZIARA BILAL MAKAO MAKUU.

Mnamo Oktoba 4, 2022 Sheikh/Dkt Murtaza Alidina alifanya ziara katika ofisi za makao makuu BMMT na kufanya mazungumzo na Mwenyekiti wa BBMT – Alhaj Husein Karim.

Katika ziara hiyo Dkt. Alidina alipata fursa ya kuona shuguli mbalimbali zinazofanywa na taasisi ya Bilal.

Dkt. Alidina ni mzaliwa wa Zanzibar, Daktari kitaaluma na ni miongoni mwa wasomi wakubwa wenye kutegemewa kutokana na ushawishi wake kwenye masuala ya kiroho.

Taasisi ya Bilal inatoa shukrani za dhati kwa Sheikh/ Dkt Alidina kwa kututembelea, tunarajia kuyatumia maelekezo yake katika kuboresha mfumo wetu wa kuihudumia jamii.

(Kushoto) Sheikh/Dkt Murtaza Alidina (Kulia) Mwenyekiti wa BMMT – Alhaj Husein Karim kwenye mazungumzo Bilal Makao Makuu.
Kushoto: Sheikh/Dkt Murtaza Alidina, Mwenyekiti wa BMMT – Alhaj Husein Karim (aliyevaa kanzu nyeusi) pembeni yake Mkuu wa Idara ta Tabligh BMMT Taifa – Sheikh Msabaha Mapinda.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *