KUMBUKUMBU YA KIFO CHA ALLAMAH SAYYID SAEED AKHTAR RIZVI 1927-2002

 KUMBUKUMBU YA KIFO CHA ALLAMAH SAYYID SAEED AKHTAR RIZVI 1927-2002

Tarehe 20/06/2002 ni siku aliyofariki dunia Mwanachuoni mkubwa wa Kiislamu wa madhehebu ya Shia Ithnaashari nchini Tanzania, Allamah Sayyid Saeed Akhtar Rizvi.

Allamah Sayyid Saeed Akhtar Rizvi, alifika nchini Tanzania mwanzoni mwa miaka ya sitini. Ilipofika mwaka 1962 Allamah Sayyid Saeed Akhtar Rizvi aliandaa mpango wa Tabligh kwa ajili ya wenyeji wa nchi ya Tanganyika kama ilivyokuwa ikijulikana hapo zamani kabla ya muungano wa Tanganyika na Zanzibar, uliyozaa Tanzania.

Mwaka 1964 Africa Federation of Khoja Shia Ithnaashari kwenye mkutano wake uliyofanyika mjini Tanga, ilipitisha azimio la kuundwa kwa taasisi ya Bilal Muslim Mission, na mnamo mwaka 1968, Bilal Muslim Mission of Tanzania ilisajiliwa rasmi Serikalini na kuanza kazi ya Tabligh chini ya uongozi wa Allaamah Rizvi.

Maamuzi haya yalifikiwa baada ya kupata ijaza au ruhusa ya marhoum Sayyid Muhsin al Hakim aliyekuwa Marja’a wa wakati huo.

Uandishi wa Vitabu

Pamoja na kazi ya Tabligh, Allaamah Sayyid Saeed Akhtar Rizvi alikuwa na kipawa cha uandishi kilicho muwezesha kuandika vitabu vingi vya aina mbalimbali.

Inakadiriwa kuwa ameandika vitabu zaidi ya 125 kuhusu mas’ala ya Aqida, Akhlaq, Sheria ya Kiislamu na Histroria ya Kiislamu.

Vitabu hivi vimechapishwa kwa lugha mbalimbali zikiwemo Kiswahili, Kiingereza, Kifursi, Kiarabu, Kihausa na Kishona.

Innaa Lillah wainnaa Ilaihi Rajiuun (Sisi wote ni milki ya Mwenyezi Mungu na kwake ndiko kwenye marejeo). Mwenyezi Mungu aipumzishe roho yake mahala pema peponi. Ameen.

Imetolewa na Kitengo cha Tabligh, The Bilal Muslim Mission of Tanzania, Jumatatu June 20, 2022 sawa na Mwezi 19 Dhul Qa’dah 1443.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *