BILAL YAADHIMISHA MAZAZI YA IMAM MAHDI (A.F.S)

 BILAL YAADHIMISHA MAZAZI YA IMAM MAHDI (A.F.S)

Vituo vya Bilal kote nchini vimefanya maadhimisho ya kukumbuka mazazi ya Imam wa zama zetu, Mahdi (a.f.s) kwa namna ya kipekee ambapo mbali na kufanya majilis mbalimbali pia michezo, hususani mpira wa miguu ilitumika kuufiksha ujumbe wa Imam.

Vituo mbalimbali vya Bilal hususani Bilal Pwani na Kusini pilianzisha ligi maalumu na kuipa jina Mahdi Cup ambayo ilikuwa njia nzuri ya kuwafikia watu hasa makundi ya vijana ambapo Bingwa alipewa zawadi ya mbuzi.

Mbali na michezo, mambo mengine yaliyofanyika vituoni ni yale yenye kuigusa jamii moja kwa moja ikiwemo kufanya usafi kwenye maeneo ya kijamii kama zahanati lakini pia kutembelea wagonjwa mahospitalini na vituo vya kulea watoto.

Kwa upande wa Bilal Comprehensive School (BCS) wao walipata heshima ya kufurahia siku hiyo kwa ugeni wa sheikh Nabil Awan wa nchini Uingereza aliyeambatana na mwenyeji wake Sheikh Syed Adil, Imam wa Masjid Khoja Dar es salaam.

Sheikh Nabil Awan alipata fursa ya kuongoza zoezi la kupandisha bendera ya Imam.

Kwa ujumla matukio haya yote yamelenga kuwakumbusha kujiandaa kumpokea Imam wa zama atakapokuja kubainisha haki na batil.

Uonhozi wa Bilal Muslim Mission of Tanzania (BMMT) unapongeza wakuu wa kanda na vituo kwa ubunifu mkubwa katika kuadhimisha mazazi ya Imam Zaman kwa mwaka huu 1443 A.H – 2022.

Bilal Arusha.
Sheikh Nabil Awan wa Uingereza akiongoza zoezi la upandishaji bendera ya Imam wakati wa sherehe za kukumbuka mazazi ya Imam Mahdi – BCS – Temeke, Dar Es Salaam.
Bilal Udoe – Ilala, Dar es salaam.
Waumini kutoka Bilal Zanzibar wakiwa na wenyeji wao kwenye dua’a maalumu walipotembea wodi ya watoto, kuwajulia hali na kuwapa zawadi katika hospitali ya Mnazi mmoja, Zanzibar.
Waumini kutoka Bilal Zanzibar wakiwa na wenyeji wao walipotembea kituo cha kulea watoto (Nyota – Zanzibar) kuwajulia hali na kuwapa zawadi.
Bilal Ikwiriri.
Mahdi Cup – Bilal Ikwiriri.
Bilal Mwanza
Mahdi Cup – Bilal Mwanza

 

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *