ZIARA YA SHEIKH NABIL NA SYED ADIL HAWZATUL BILAL – TEMEKE, DAR ES SALAAM.

 ZIARA YA SHEIKH NABIL NA SYED ADIL HAWZATUL BILAL – TEMEKE, DAR ES SALAAM.
Kutoka kushuto kwenda kulia: (Mbele) Sheikh Nabil Awan, Alhajj Hussein Karim. (Nyuma) Sheikh Muhammad Yusuph, Sheikh Syed Adil.

Sheikh Nabil Awan, Imam kutoka nchini Uingereza akiambatana na Sheikh Syed Adil, Imam wa Masjid Khoja Dar es salaam walifanya ziara katika Hawza ya Bilal iliyopo Temeke Dar es salaam.

Ziara ya wawili hao ililenga kuangalia maendeleo ya Tabligh na hali ya masomo kwa ujumla katika hawza hiyo.

Ziara hiyo ilifanyika Alkhamis ya tarehe tarehe 17 March 2022 sawa na 14 Shaaban 1443 A.H ambapo wageni waliambatana na wenyeji wao kutoka Bilal Makao akiwemo Mwenyekiti – Alhajj Hussein Karim, Afisa Mtendaji Mkuu – Ndugu Hafidh Mansour.

Mambo mbalimbali yalifanyika wakati wa ziara hiyo ikiwemo wageni kuonana na wanafunzi, na uongozi wa Hawza.
Wawili hao wamefurahishwa na harakati za kitabligh zinazofanywa kwenye hawza hiyo.

Uongozi wa Bilal unawashukuru Sheikh Nabil Awen na Sheikh Syed Adil kwa kufanya ziara hiyo na inawaombea kwa Mwenyezimungu waendelee kuwa na afya njema.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *