BMMT KATIKA IFTAR YA PAMOJA | RAMADHAN 2023

 BMMT KATIKA IFTAR YA PAMOJA | RAMADHAN 2023

 

Uongozi wa Bilal Muslim Mission of Tanzania (BMMT) ukiongozwa na mwenyekiti wake, Alhaj Hussein Karim, umefanya hafla fupi ya iftar ya pamoja na kuwakutanisha, viongozi wa bodi, watendaji, viongozi wastaafu, na wageni waalikwa wakiwemo wa taasisi ya Africa Federation (AFED).

Hafla hiyo fupi ilifanyika terehe 29 March, 2023 sawa na mwezi 7 Ramadhan, 1444 A.h katika ukumbi wa mafunzo uliopo kweye ofisi za makao makuu ya AFED jijini Dar es salaam na ilipata heshima ya kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali akiwemo Alhaj Aunali Khalfani – Makamo Mwenyekiti wa AFED aliyeambatana na viongozi waandamizi kadhaa wa AFED.

Makamo M/kiti wa AFED, Alhaj Aunali Khalfan (aliyesimama) akizungumza wakati wa hafla ya iftar iliyoandaliwa na BMMT Makao Makuu| Picha na Idara ya habari 29 March, 2023.

Wengine waliohudhuria kutoka BMMT ni pamoja na Alhaj AbdulWahid Mohammed – Makamo Mwenyekiti, Alhaj Mohamedraza Barwani – Katibu, Hafidhi Mansour – Afisa Mtendaji Mkuu, Alhaj HusseinAziz Rajani – Mwenyekiti wa BMMT kanda ya Pwani & Kusini, Sheikh Msabaha Mapinda – Mkuu wa Idara ya Tabligh, Sheikh Mohammad Yusupu – Mudeer Hawzatu Bilal – Temeke pamoja na watendaji wengine kutoka idara mbalimbali.

PICHA ZA MATUKIO MBALIMBALI

Pamoja na tukio la iftar, palikuwa na mazungumzo mafupi kutoka kwa Alhaj AbdulWahid Mohammed na Alhaj Aunali Khalfan ambapo wahudhuriaji walipata fursa ya kutambua juhudi iliyofanyika katika kuzijenga taasisi za BMMT na AFED vilevile kujadili namna ya kuendeleza harakati za taasisi hizi.

Huu ni utamaduni wa kawaida kwa BMMT kuandaa hafla kama hii mara moja kila inapofika Ramadhan, malengo ni kutambuana, kubadilishana uzoefu hususani katika namna ya kuimarisha harakatai za taasisi zetu.

Kwa niaba ya Uongozi wa BMMT, tunapenda kutoa shukrani kwa uongozi wa AFED na wote waliofanikiwa kuhudhuria katika hafla hiyo na tunataraji kuwa tutaenelea kushirikiana katika harakati mbalimbali za kumtumikia imam wa zama zetu, Imam Muhammad Mahdi (a.t.f.s).

Wafanyakazi wa BMMT na wageni waalikwa kwenye picha ya pamoja baada ya hafla ya iftar iliyoandaliwa na taasisi hiyo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *