BMMT KISHURO – KAGERA YAPOKEA MRADI WA VYUMBA VIWILI VYA MADRASA

 BMMT KISHURO – KAGERA YAPOKEA MRADI WA VYUMBA VIWILI VYA MADRASA

Bilal Muslim Mission of Tanzania (BMMT) imekamilisha ujenzi wa madrasa katika kituo cha Kishuro kilichopo Kijiji cha Kishuro, kata ya Ngenge, Wilayani Muleba mkoani Kagera.

Hafla ya makabidhiano ya mradi huo ilifanyika February 26, 2023 na ilihudhuriwa na msimamizi wa kanda ya Kagera (Bukoba) Sheikh Maftah Omary Maftah, Alhaj Amiraly Datoo, waumini na wanafunzi.

Mradi huu uliojumuisha ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa, vyoo, na madawati ulianza mwishoni mwa December, 2022 na kukamilika January 2023 na ulifadhiliwa na Alhaj Amiraly Datoo na timu yake.

Mradi huu unaenda kuwanufaisha wanafunzi 48 wa madrasa ambao awali walikuwa wakisoma chini ya mti. Pamoja na kukabidhi mradi huo, Alhaj Datoo pia alitoa zawadi ya chakula ikiwa pamoja na unga wa sembe, sukari, maharage, na nyama vingine ni vyombo, mikeka, Mas-haf na Juzuu.

Alhaji Datoo na timu yake wamekuwa wakiunga mkono harakati nyingi za BMMT hususani katika mkoa wa Kagera na msaada wao umekuwa kwenye maeneo ya ugawaji wa Mas-haf, vitabu, chakula, ukarabati wa madarasa, uchimbaji wa visima na nambo mengine kadhaa ambayo yanamsaada mkubwa katika kuinua hali za maisha za watu katika mkoa wa Kagera.

Mwonekano wa ndani wa vyumba vya madarasa (madrasa)
Mstari wa mbele kutoka kushoro kuelekea kulia: Msimamizi wa vituo BMMT kanda ya Kagera (Bukoba)- Sheikh Maftah Omary Maftah akifuatiwa na Alhaj Amiraly Datoo kwenye picha ya pamoja na waumini wa Kishuro…

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *