UONGOZI WA BILAL MUSLIM MISSION TANZANIA UMEKUTANA NA WASIMAMIZI WA VITUO.

Uongozi wa juu wa Bilal Muslim Mission of Tanzania (BMMT) ukiongozwa na Mwenyekiti Alhaj Hussein Karim, Makamo Mwenyekiti Alhaj Abdul-Wahid Mohammed na Afisa Mtendaji Mkuu Alhaj Hafidhi Mansour walikutana na viongozi wa kanda kujadili namna ya kuongeza ufanisi katika utekelezaji wa majuumu ya kila siku katika vituo.
Mkutano huo ulifanyika Jumatatu ya December 12, 2022 katika ofisi za Africa Federation (AFED Tower) jijini Dar es salaam. Mkutano huo ulipata heshima ya kuhudhuriwa na Makamo Mwenyekiti wa AFED, Alhaj Aunali Khalfan.
Wengine walioshiriki katika mkutano huo ni pamoja na Mwenyekiti wa BMMT Kanda ya Pwani & Kusini, Alhaj Aziz Hussein Rajani, na wasimamizi wa kanda kutoka Mwanza, Kigoma, Pwani & Kusini, Kagera, Zanzibar, Pemba, Tabora, Singida, Moshi, Rwanda na Malawi.

Pembezo mwa mkutano huo, washiriki walipata fursa ya kujifunza historia ya AFED na kuona namna taasisi hiyo kubwa inavyofanya shuguli zake.


Tunaamini kwamba mkutano huu utaleta matokeo chanya na kuongeza ufanisi katika kumtumikia imam wa zama zetu, Imam Muhammad Mahdi (a.f.s).