BMMT KANDA YA PWANI & KUSINI YAANDAA SEMINA YA MWISHO WA MWAKA 2022.

 BMMT KANDA YA PWANI & KUSINI YAANDAA SEMINA YA MWISHO WA MWAKA 2022.

Bilal Muslim Mission of Tanzania (BMMT) kanda ya Pwani & Kusini iliandaa semina ya wiki moja kwa Muballighina, semina iliyolenga kuwaongezea uwezo Mubalighina.

Semina hiyo ilifanyika Hawzatu Bilal, Temeke kuanzia December 05 – 11, 2022 ambapo mada mbalimbali ziliwasilishwa ikiwemo; masuala ya Uongozi, Maadili, Sharia, Mahusiano ya umma na kadhalika.

Uongozi wa BMMT ukiongozwa na Mwenyekiti wake Husein Karim (eatano kutoka kushoto) wakati wa semina)

Semina hii ilipata heshima ya kuhudhuriwa na viongozi waandamizi wa BMMT akiwemo Mwenyekiti, Haj Hussein Karim; Makamo Mwenyekiti, Haj Abdul-Wahid Mohammed; Mtendaji Mkuu, Haj Hafidh Mansour; Mwenyekiti BMMT Kanda ya Pwani & Kusini, Haj AzizHussein Rajani, Mkuu wa Tabligh Taifa, Haj Msabaha Mapinda na Mtendaji Mkuu wa The Mainstay Foundation Haj Amir Taqi.

Wengine ni Wasimamizi wa vituo kutoka Kanda mbalimbali wakiongozwa na mwenyeji wao wa kanda ya Pwani na Kusini Sheikh Swahibu Rashid.

Mtendaji Mkuu wa The Mainstay Foundation Haj Amir Taqi (Aliyevaa shati la buluu bahari) kwenye picha ya pamoja na washiriki wa semina.

Katika siku ya mwisho ya semina, washiriki wote walipatiwa vyeti na kupata fursa ya kuzuru na kufanya dua kwenye kaburi la Muasisi wa BMMT Allamah Sayyid Saeed Akhtar Rizvi.

Wasimamizi wa vituo kutoka kanda mbalimbali walipozuru na kufanya dua kwenye kaburi la muasisi wa BMMT, Allamah Sayyid Saeed Akhtar Rizvi.
Waalimu wa vituo vya kanda ya Pwani & Kusini walipozuru na kufanya dua kwenye kaburi la muasisi wa BMMT, Allamah Sayyid Saeed Akhtar Rizvi.

Tunaamini kuwa, semina hii imewaongezea maarifa makubwa Muballighina wetu na inaenda kuwaongezea ufanisi katika utekelezaji wa majukumu yao ya kila siku katika kuihudumia jamii.

BMMT Makao Makuu inatoa pongezi kwa Uongozi wa BMMT kanda ya Pwani & Kusini kwa maandalizi ya semina hii pia inatoa shukrani kwa washiriki wote wakiwemo kutoka Mwanza, Tanga, Singida, Zanzibar, Mtwara na kila mmoja kwa nafasi yake waliochangia kufanikisha semina hii. Mwenyezi Mungu atawalipa zaidi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *