Sauti ya Bilal | Online Radio

SHEREHE ZA MAULID ZA BILAL MUSLIM MISSION OF TANZANIA (BMMT) – 1444 A.H (2022)

 SHEREHE ZA MAULID ZA BILAL MUSLIM MISSION OF TANZANIA (BMMT) – 1444 A.H (2022)

Tarehe 5 Novemba 2022, Bilal Muslim Mission of Tanzania (BMMT) ilifanya sherehe za Maulid ya Mtume Muhammad (s) katika viwanja vya chuo cha Bandari karibu na Hawzatu Bilal – Tandika.

Mgeni rasmi katika hafla hiyo alikuwa Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar Es Salaam, Sheikh Alhadi Musa Salum. Hafla hiyo pia ilihudhuriwa na balozi wa Iran nchini Tanzania, Hossein Alvandi Behineh na ujumbe wake; Mwenyekiti Central Bilal Board (CBB), Alhaj Mohamed Hemani; Mwanzilishi wa taasisi ya WIPAHZ, Alhaj Haji Saheb; Mwenyekiti Bilal Tanzania, Alhaj Hussein Karim; Makamu Mwenyekiti wa Bilal, Alhaj Abdul-Wahid Abdallah Mohamed; Afisa Mtendaji Mkuu wa Bilal Tanzania, Ndugu Hafidh Mansour; Mkuu wa Tabligh BMMT, Sheikh Msabaha Shaban Mapinda; Sheikh/Daktari Abdul-Razaq Amir; Bilal Hawza Mudeer, Sheikh Mohammad Yusuph; na Wasimamizi wa Tabligh kutoka kanda mbalimbali.

Zaidi ya watu 1000 kutoka maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es Salaam na maeneo ya jirani zikiwemo madrasa mbalimbali kutoka kwa ndugu zetu wa madhehebu ya Sunni walihudhuria hafla hiyo.

Wazungumzaji walipata fursa ya kuhutubia wananchi wakiunganisha hotuba zao na kaulimbiu ya mwaka huu isemayo “kusimamia maadili ni jukumu letu sote” huku Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Sheikh Alhadi Musa Salum akitumia jukwaa hilo kuwatolea wito Waislamu kote Tanzania, kuimarisha umoja baina yao.

BMMT, inapenda kuwashukuru wageni wote kwa kuhudhuria hafla hiyo, pia inatoa shukrani za dhati kwa wafadhili wa hafla hiyo, viongozi na wajumbe wa kamati na kila mmoja kwa nafasi yake kwa kufanikisha hafla hii muhimu.

_DSC9635
_DSC9666
_DSC9688
_DSC9740
_DSC9747
_DSC9777
previous arrow
next arrow
Play Video
Play Video
Play Video

Tukio kama hilo pia limefanyika katika vituo vingine vya Bilal kote nchini kwa nyakati tofauti. 

Mbali na Majalis, baadhi ya vituo vilitumia michezo kufikisha ujumbe wa Mtume Muhammad (s) kwa umma.

BMMT SUMBAWANGA

Kwa mara nyingine tena, BMMT inapenda Kumshukuru kila mmoja kwa kuhudhuria, pamoja na wafadhili na wote waliofanikisha hafla hizi. 

Imetayarishwa na: 

Idara ya Habari na Mahusiano ya Umma

Bilal Muslim Mission of Tanzania (BMMT)

Makao Makuu – Dar es salaam.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *