RAIS WA KHAKI FOUNDATION AFANYA ZIARA BILAL MAKAO MAKUU.

 RAIS WA KHAKI FOUNDATION AFANYA ZIARA BILAL MAKAO MAKUU.

Rais wa Khaki Foundation ndugu Jawad Khaki amefanya ziara katika ofisi za makao makuu ya Bilal Muslim Mission of Tanzania (BMMT) zilizopo mtaa wa Libya – Ilala, jijini Dar es salaam na kujionea namna taasisi hiyo kongwe nchini inavyofanya shuguli zake.

Amefanya ziara hiyo mnamo Oktoba 5, 2022 ambapo pamoja na mambo mengine alipata fursa ya kutembelea ofisi za idara mbalimbali za taasisi hiyo na kujifunza namna wanavyofanya majukumu yao ya kila siku pia alipata fursa ya kuzungumza na uongozi wa BMMT ukiongozwa na Mwenyekiti Alhaj Husein Karim.

Khaki ni mfanyabiashara na Mhisani ambaye kwa kushirikiana na mke wake Khaniz walianzisha taasisi ya Khaki Foundation mnamo mwaka 2003 kwa lengo la kusaidia wanajamii walio hatarini zaidi hususani kwenye nyanja ya elimu ili kukabiliana na umasikini. Pia alikuwa Makamu wa Rais wa kampuni ya Microsoft kwa zaidi ya miaka 20.

Taasisi ya Bilal inatoa shukrani za dhati kwa ndugu Jawad Khaki kwa kututembelea, tunarajia kuyatumia maelekezo yake katika kuboresha mfumo wetu wa kuihudumia jamii na pia tunazamaia kushirikiana katika mambo mbalimbali kwa siku usoni In sha Allah.

Kutoka kushoto: Mwenyekiiti wa BMMT – Husein Karim, Rais wa Khaki Foundation – Jawad Khaki, Afisa Mtendaji Mkuu wa BMMT – Hafidh Mansour
Rais wa Khaki Foundation – Jawad Khaki, akimwelekeza jambo Mhasibu Mwandamizi wa BMMT – Dada Fatemah Kermali.
Kutoa kushoto: Mwenyekiti wa BMMT – Husein Karim, Rais wa Khaki Foundation – Jawad Khaki akielezewa jambo na Mkuu wa Tabligh (Kanda ya Pwani & Kusini) Sheikh Swahib Rashid.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *