SEMINA ELEKEZI KWA MUBALLIGHINA WAPYA


Alhamdullillah, kwa neema ya Mwenyezi Mungu Taasisi ya Bilal Muslim Mission of Tanzania (BMMT) ikiwa Hawzatu Bilal, imefanikiwa kuendesha semina elekezi ya siku moja kwa Muballighina wapya ambao wanatarajiwa kuanza kazi kwenye vituo walivyopangiwa haraka iwezekanavyo.
Semina hiyo ililenga kuwapa nasaha Mubalighina juu ya Akhlaq (Tabia njema), kutoa maelekezo juu ya wajibu na majukumu ya Muballighina na namna ya kutekeleza kazi zao za kila siku kulingana na sera na miongozo ya Taasisi.
Semina hiyo ilihudhuriwa na viongozi mbalimbali wa bodi akiwemo Mwenyekiti wa Bilal Ndugu Hussein Kareem, Makamo Mwenyekiti Alhajj Abdul-Waheed Zakaria, Mwenyekiti wa Bilal kwa vituo vya Pwani na Kusini Ndugu Azizi Hussein, na Mkuu wa Kitengo cha Tabligh Bilal Sheikh Msabaha Mapinda.
Wengine ni Mkuu wa Utawala katika vituo vya Bilal Pwani na Kusini Ndugu Sinani Kamegi, Mdiru wa Hawzatu Bilal Sheikh Muhammad Yusuph, Katibu wa Tabligh (BMMT) Sheikh Abdul – Azizi Atiki na masheikh wengine wa Hawza, pia Semina hii ilipata heshima ya kuwa na masheikh waalikwa ambao ni miongoni mwa masheikh wa mwanzo kabisa wa Bilal na wanafunzi wa Marhoum Allamah Sayyid Saeed Akhtar Rizvi. Masheikh hao ni Sheikh Ramadhani Kwezi pamoja na Sheikh Hassan Ndimbo.
Semina pia ilijumuisha wazungumzaji wengine akiwemo Msimamizi wa Vituo vya Bilal Mwanza Sheikh Hassan Muhidin aliyeshiriki kwenye semina moja kwa moja kupitia mtandao (Sykpe).
Chini ni picha mbalimbali kutoka kwenye semina hiyo…








- Bofya link https://youtu.be/9Pw8bbZAgqc?t=2 kuona na kusikiliza nasaha za M/Kiti wa BMMT Ndugu Hussein Kareem kwa Muballighina wapya
- Bofya link https://www.youtube.com/watch?v=4VwevYitZEw&t=136s kuona na kusikiliza nasaha za Makamo M/Kiti wa BMMT Alhajj Abdul-Wahid Zakaria kwa Muballighina wapya
- Bofya link https://www.youtube.com/watch?v=BgKqum6-BcQ kuona na kusikiliza nasaha (ujumbe) wa Mkuu wa Tabligh wa BMMT Sheikh Msabaha Mapinda kwa Muballighina wapya
- Bofya link https://www.youtube.com/watch?v=I_oGvhWIyjE kuona na kusikiliza nasaha (ujumbe) wa Mdiru wa Hawzatu Sheikh Muhammad Yusuph kwa Muballighina wapya