BILAL COMPREHENSIVE SCHOOL ANNUAL DAY (2021)

 BILAL COMPREHENSIVE SCHOOL ANNUAL DAY (2021)

Tukiwa tunaelekea kwenye kufunga mwaka wa masomo 2021, ni fursa ya kutambua kazi kubwa iliyofanywa na wanafunzi pamoja na waalimu wao katika kipindi chote cha mwaka kupitia tukio maalumu la Annual Day.

Kwa neema ya Mwenyezi Mungu tumefanikiwa kufanya tukio hili kubwa katikati ya wiki hii tunayoenda kuimaliza, ambapo awali lilihusu wanafunzi wa elimu ya awali (Nursery na Pre-Primary) ambapo pia siku hiyo imetumika kuwapongeza kwa kuhitimu masomo yao tayari kwa kuingia darasa la kwanza katika mwaka ujao wa masomo.

Baadae palifanyika hafla hii kwa wanafunzi wa elimu ya msingi (Lower Primary – Darasa la kwanza hadi la tatu & Upper Primary – Darasa la nne hadi la saba).

Shukrani za kipekee kwa Mrs. Lillian Mrema aliyekuwa mgeni rasmi kwenye tukio la kufunga mwaka na mahafali kwa wanafunzi wa elimu ya awali (Nursery & Pre-Primary), Mrs. Mayasa Mtonga aliyekuwa mgeni rasmi kwenye tukio la kufunga mwaka kwa wanafunzi wa madarasa ya awali elimu ya msingi (Darasa la kwanza hadi la tatu) na Mr. Ibrahim Mwita aliyekuwa mgeni rasmi kwenye tukio la kufunga mwaka kwa wanafunzi wa madarasa ya juu elimu ya msingi (Darasa la nne hadi la saba), wote kutoka Wizara ya Elimu.

Wazazi na walezi ni miongoni mwa waliohudhuria hafla hii, ulikuwa ni wakati muhimu wa kuona vipaji vya watoto kwenye mambo mbalimbali ikiwemo umahiri wa kusoma Qur-an, kuongea lugha ya kiingereza, na kuonesha namna watoto wanavyojiamini na kuwweza kufanya vizuri wanapopewa nafasi.

Kwa niaba ya uongozi wa shule na taasisi kwa ujumla, tunatoa shukrani za kipekee kwa wahisani wetu, Mwenyezimungu awazidishie…

Bofya link https://youtu.be/YLYf7ewxqCw kuona sehemu ya tukio hilo (video)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *