KUMBUKUMBU YA KUZALIWA IMAM ALI BIN ABI TALIB (A.S) – KWENYE VITUO VYA BILAL

 KUMBUKUMBU YA KUZALIWA IMAM ALI BIN ABI TALIB (A.S) – KWENYE VITUO VYA BILAL

Tupo katika mwezi mtukufu wa Rajab, mwezi ambao una tarehe nyingi za muhimu ikiwemo kumbukumbu ya kuzaliwa Imam Ali bin Abi Talib (a.s) aliyezaliwa tarehe 13 Rajab, 600 AD. Imam Ali (a.s) ama Amirul Mu’uminin kwa heshima, ni imam wa kwanza katika mtiririko wa maimamu 12 baada ya Mtume Muhammad (s.a.w.w).

Imekuwa ni kawaida ya Taasisi ya Bilal Muslim Mission of Tanzania kufanya majalis mbalimbali zenye mlengo wa kuweke kumbukumbu muhumu za Maasumin ikiwemo siku zao za kuzaliwa na kufariki ambayo mbali na kutunza historia ya masiku hayo muhimu pia inatoa fursa ya kuyatafakari maisha yao.

Chini tumeweka picha kutoka vituo mbalimbali vya Bilal vilivyofanya sherehe za kukumbuka kuzaliwa kwa Imam Ali (a.s)

MOSHI – KILIMANJARO (FEB 13, 2022)

Majalis imewahusisha viongozi wa kituo, pamoja na waumini wao na wageni kutoka maeneo tofauti tofauti ya Moshi mkoani Kilimanjaro.

 

   

 HAWZATU BILAL – TEMEKE, DAR ES SALAAM (FEB 15, 2022)

Majalis imeongozwa na Waalimu wa hawza hiyo waliokuwa pamoja na wanafunzi wao.

Pamoja na mambo mengine ikiwemo ufunguzi wa majalis kwa kisomo cha Qur-an, Qaswida mbalimbali, wanafunzi walipata fursa pia ya kuonesha ni kwa namna gani wamemuelewa Imam Ali (a.s) pamoja na athari ya maisha yake kwa umma wa sasa…

 

 

Bofya link https://youtu.be/Uba4b0DdWCg?t=2 kutazama namna Majalis ilivyokwenda.,

MSATA – PWANI (FEB 15, 2022)

Hafla hii ilihudhuriwa na Viongozi wa Kituo na waumini wao ikiwa pamoja na wanafunzi huku ikipata heshima ya kuhudhuriwa na Msimamizi na Mkaguzi wa Vituo vya Bilal Pwani na Kusini Sheikh Swahib Rashid aliyekuwa mgeni rasmi na mzungumzaji mkuu.

MBOGA – PWANI (FEB 15, 2022)

Hafla hii ilihudhuriwa na Viongozi wa Kituo na waumini wao ikiwa pamoja na wanafunzi, mzungumzaji akiwa ni Sheikh Yusuph Ally ambae hotuba ilijikita katika kuangalia ni kwa namna gani tunaweza kufaidika na mazazi ya Imam Ally bin Abi Talib.

………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………..

Kupata wasifu wa Imam Ali (a.s) kwa ufupi bofya link https://drive.google.com/file/d/1P9ujJ4pmBwXdDnJoxp664SP6HarNfKPc/view?usp=sharing

Kuangalia mawaidha ya Sheikh Swahib Rashid kuhusu mambo nane (8) aliyoyataja Imam Ali (a.s) kama sababu za Dua’a kutojibiwa bofya link https://youtu.be/nClb4zNgxhw?t=300

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *