MILAD-UN-NABI HAWZATU BILAL

Alhamdullillah, kwa neema ya Mwenyezi Mungu Taasisi ya Bilal Muslim Mission of Tanzania (BMMT) imefanikiwa kufanya Sherehe Maalumu ya kumbukumbu ya kuzaliwa kipenzi chetu, Mtukufu Mtume Muhammad (s.a.w.w).

Sherehe hizo zimefanyika Hawzatu Bilal, Temeke Dar es salaam na kuhudhuriwa na wakuu wa bodi, Mgeni rasmi Sheikh Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam akituma mwakilishi wake, Madrasa mbalimbali zikiwemo Madrasatul Mukhliswina, Madrasatul Aqswa, Madrasatul Azhar Sharif, Madrasatul Minhaj Twalibin, Madrasatul Saqina ambao walishiriki moja kwa moja ikiwa pamoja na usomaji wa milango.
Sehemu ya wahudhuriaji pia ilitokana na waumini wangine wake kwa waume kutoka maeneo mbalimbali ya Dar es salaam na maeneo ya jirani. Sherehe hizi ni za kawaida na zinafanywa na watu mbalimbali kutoka jamii ya Kiislamu, malengo ikiwa kuzitaja sifa za mtukufu Mtume (s.a.w.w) na kutoa fursa kwa waumini wa kiislamu kuyatafakari maisha na matendo ya bwana mtume (s.a.w.w) na kisha kuyaingiza katika maisha yetu ya kila siku.
Hata hivyo Sherehe hizi zimefanyika kwa mara ya kwanza Hawzatu Bilal, hivyo zimetoa funzo kutokana na changamoto kadhaa zilizojitokeza, tunatarajia sherehe hizi kuwa bora zaidi kwa miaka ijayo. Kwa upekee tunatoa shukrani kwa wote walioacha shuguli zao na kushiriki kwenye tukio hili kubwa kabisa na pia shukrani za dhati kwa wahisani waliotushika mkono na kufanikisha kufanyika kwa shuguli hii kupitia michango yao mbalimbali…
CHINI: SEHEMU YA MATUKIO YA MAULID KWA PICHA









