Office Hours
Mon-Fri: 08:30am-05:30pm Saturday: 08:30am-01:30pm

Majlis za Muharram Zaendelea Kuvuta Mamia ya Waumini katika Vituo vya Bilal Muslim Mission of Tanzania.

Waumini wa Ahlul-Bayt (A.S.) katika vituo mbalimbali vya Bilal Muslim Mission of Tanzania wanaendelea kushiriki majlis za Muharram zinazofanyika katika maeneo tofauti nchini ikiwa ni sehemu ya kuenzi na kuhuisha ujumbe wa Karbala.

KAULI MBIU YA MWAKA HUU NI; KARBALA SOMO LA UADILIFU,UMOJA NA HUDUMA KWA JAMII.

Katika kipindi hiki cha maombolezo, vituo vya taasisi vimeendelea kuendesha shughuli mbalimbali za kidini na kielimu zikiwemo majlis za Nahasa, mihadhara ya dini, usomaji wa Qur’an Tukufu, dua pamoja na vipindi vya maswali na majibu. Programu hizi zimewaweka pamoja waumini wa rika mbalimbali kujifunza na kutafakari mafunzo yanayotokana na maisha na kujitoa kwa Imam Hussein (A.S.) na wafuasi wake katika tukio la Karbala.

Muharram ni kipindi muhimu katika kalenda ya Kiislamu kinachokumbusha misingi ya haki, uadilifu, subira na kujitolea kwa ajili ya dini. Kupitia majlis hizi, waumini wanapata fursa ya kujifunza namna ya kuendeleza maadili hayo katika maisha yao binafsi na katika jamii kwa ujumla.

 

 

 

 

 

 

 

Bilal Muslim Mission of Tanzania inaendelea kuwashukuru viongozi vya vituo, waumini, wadau na wafadhili wote wanaoshiriki na kuunga mkono programu hizi katika vituo mbalimbali vya taasisi. Ushiriki wao umechangia kuendelezwa kwa ujumbe wa Karbala na kuimarisha shughuli za kiroho katika jamii.

Taasisi inawakaribisha waumini na jamii kwa ujumla kuendelea kushiriki katika majlis na shughuli mbalimbali zinazoendelea katika siku hizi za Muharram.

Picha za vituo mbalimbali vikiadhimisha siku 10 za mwenzi Muharram.

 

 

 

 

 

 

 

 

About the Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

You may also like these

{title}