Office Hours
Mon-Fri: 08:30am-05:30pm Saturday: 08:30am-01:30pm

TAARIFA KWA UMMA

Assalaam Alaykum Warahmatullahi Wabarakaatuh.

Taasisi ya Bilal Muslim Mission of Tanzania inautaarifu umma, vyombo vya habari, na jamii kwa ujumla kuhusu uwepo wa Maadhimisho Maalum ya kihistoria linalotarajiwa kufanyika hivi karibuni jijini Dar es Salaam. Maadhimisho haya ni sehemu ya jitihada endelevu za taasisi katika kujenga uelewa mpana wa kuimarisha mshikamano, na kujadili mustakabali wa jamii.

Maadhimisho haya yanalenga hasa vijana (wakike na wakiume) kuanzia umri wa miaka 15 na kuendelea, ambao ni nguvu kazi na mustakabali wa Ummah.

 

Mada Kuu: “GHADIR; UJUMBE WA UONGOZI NA MUSTAKABALI WA UMMA”.

Tukio hili limeandaliwa kwa lengo la kuelimisha na kuwakumbusha waumini, hasa kizazi kipya kuhusu umuhimu na uzito wa tukio la Ghadir katika historia ya Uislamu.Aidha, kupitia maadhimisho haya yatachambua kwa kina nafasi ya ujumbe huo katika kuwajengea vijana uwezo wa uongozi, pamoja na kuimarisha umoja, uelewa wa pamoja, na mshikamano thabiti wa Ummah wa Kiislamu katika kukabiliana na changamoto za sasa na za baadaye.

Ratiba na Mahali madhimisho yatafanyika:

Siku: Jumapili

Tarehe: 07, Juni 2026

Muda: Kuanzia saa 2:30 Asubuhi hadi saa 10:00 Jioni

Mahali: Ukumbi wa Unit Hall – WIPAHS, Chang’ombe, Temeke, Dar es Salaam.

Taasisi inakaribisha wadau wote na jamii kujumuika katika kufanikisha adhimisho hili.

Kwa muongozo au ufafanuzi, tafadhali wasiliana nasi kupitia:Simu: +255 675 772 595 & 0745 111 150.Tunatanguliza shukrani za dhati kwa utayari wenu. Mwenyezi Mungu (SWT) awalipe kheri, awabariki afya njema, na ajaalie mafanikio katika kila hatua.

Wabillahit Tawfeeq.

Kb:Chakula na Usafiri vitatolewa bure

Taarifa hii imetolewa na Kitengo cha Habari na Uhusiano,

Bilal Muslim Mission of Tanzania.

About the Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

You may also like these

{title}