Ugawaji wa chakula Ramadhan 1444 Hijiria | 2023.

 Ugawaji wa chakula Ramadhan 1444 Hijiria | 2023.

Zaidi ya kaya 5833 zilinufaika kwenye mpango wa ugawaji chakula wakati wa mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhan mwaka 2023 sawa na mwaka 1444hijiria.

Mpango huu umetekelezwa kuanzia mwishoni mwa mwezi wa Sha’ban na mwanzoni mwa mwezi wa Ramadhan huku wanufaika wakiwa waumini kutoka vituo mbalimbali vilivyo chini ya usimamizi BMMT, taasisi binafsi, na watu binafsi (wahitaji).

Mbali na makundi hayo, wengine waliofikiwa na mpango huu ni kundi la watoto yatima ambapo jumla ya vituo tisa vilifikiwa.

Vitu vilivyotolewa mwaka huu ni pamoja na mchele, unga wa ngano,
unga wa sembe, maharage, sukari, mafuta ya kula, tambi, tende na chumvi ambazo ni miongoni mwa bidhaa muhimu katika msimu wa Ramadhan.

Mpango huu ni mahususi kwa ajili ya kupunguza makali ya gaharama za maisha zinazotokana na kupanda kwa bei katika bidhaa za chakula hususani kila unapofika msimu wa mwezi mtukufu wa Ramadhan.

Bilal Muslim Mission of Tanzania (BMMT) imetekeleza mradi huu kwa kushirikiana na The Mainstay Foundation – UK, Imam Hasan Foundation – Australia, Africa Federation (AFED), Masters Foundation na Jan Mohammed Family.

 

MATUKIO KATIKA PICHA BAADHI YA MAENEO

SONY DSC

      

SONY DSC
SONY DSC
SONY DSC

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *