Takriban watoto yatima 385 wapata zawadi za Eid ul Fitr 2023 | 1444 AH

 Takriban watoto yatima 385 wapata zawadi za Eid ul Fitr 2023 | 1444 AH

Bilal Muslim Mission of Tanzania (BMMT) kwa kushirikiana na The Mainstay Foundation, UK wametoa zawadi za nguo kwa takriban watoto 385 kwa ajili ya kusherehekea sikukuu ya Eid ul Fitr 2023 (1444 AH).

Zawadi hizo zimetoloewa katika tarehe tofauti tofauti kwenye kumi la mwisho la mwezi mtukufu wa Ramadhan, 1444 AH katika vituo mbalimbali vya kulea watoto yatima kwenye mikoa ya Tabora, Kagera, Mwanza na Dar es salaam.

Zawadi zilizotolewa ni fulana na suruali (jeans) kwa wavulana na gauni kwa wasichana na hivyo kutengeneza faraja kwao katika kipindi cha sikukuu.

MATUKIO KATIKA PICHA BAADHI YA VITUO

                                      

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *