MUHAMMAD NABII WA MWISHO – PAKUA SASA…

 MUHAMMAD NABII WA MWISHO – PAKUA SASA…

Moja katika ya Mizizi (Msingi/Itikadi) ya dini ya Kiislamu ni kuamini juu ya uwepo wa Manabii ambao ni wajumbe wa Mwenyezi Mungu hapa Ulimwenguni. Kwa ujumla wake kuna manabii 124,000 wakianziwa na Adam (a.s) hadi Mtume Muhammad (s.a.w.w).

Lakini kutokana na tofauti za dini na madhehebu kumekuwa na kutokubaliana juu ya nafasi ya manabii hao, wapo ambao wanaamini kuwa nabii Isa (a.s) ndie wa mwisho na hakuna tena nabii badala yake, wapo wanaomini kuwa yupo nabii mwingine baada ya Mtume Muhammad.

Mwenyezi Mungu anasema, “Nasi Hatukukutuma ila uwe rehema kwa walimwengu.” (Qur an – 21:108). Maneno haya ni ya Mwenyezi mmungu mwenyewe kwa Mtume Muhammad ambayo yanabainisha kuwa Muhammad (s.a.w.w) si mtume wa waislam tu bali wa ulimwengu mzima.Kwenye hiki patachambuliwa hoja mbalimbali juu ya imani ya kuwa Muhammad (s.a.w.w) ndiye nabii wa mwisho wa Mwenyezi Mungu na nini khatma ya Ulimwengu baada yake…

Bofya link https://drive.google.com/file/d/1kq2AOv6PqVsKSlzMQw6sTpNSuck_ZSdO/view?usp=sharing kupakuwa

Kitabu hiki kimeandikwa na Allamah Sayyid Saeed Aktar Rizvi na kutarjumiwa na Maalim Dhikiri Kiondo na kilitoka kwa mara ya kwanza mnamo mwaka 1978 kikiwa na ISBN NO. 9987 620 23 X

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *