DAR ES SALAAM – TANZANIA – Katika kuelekea msimu wa sikukuu ya Eid al-Adha, The Bilal Muslim Mission of Tanzania, imetangaza rasmi kuanza kwa kampeni ya Qurbani 2026. Kampeni hii inalenga kuwasaidia waumini kutekeleza ibada hii muhimu kwa ufanisi, huku ikihakikisha kuwa kutoa huko kunaleta tija ya moja kwa moja kwa jamii zenye uhitaji nchini kote.
Changamoto kubwa wakati wa msimu wa Qurbani ni kuhakikisha kuwa ibada inatekelezwa kwa kufuata misingi ya kidini (Halal) na kwamba nyama inawafikia walengwa walio masikini na wenye uhitaji wa kweli. Bilal Muslim Mission inaziba pengo hilo kwa kuratibu zoezi zima kuanzia ununuzi wa mnyama mpaka ugawaji.
Qurbani ni zaidi ya kutoa mnyama; ni kielelezo cha utii uliotukuka na moyo wa ukarimu. Kama ilivyoandikwa, si nyama wala damu inayomfikia Allah, bali ni uchamungu na nia ya dhati ya mtoaji. Kupitia ukarimu wako leo, unajenga akiba ya kudumu kwa ajili ya kesho yako.
Picha ikielezea mchakato na utaratibu wa utoaji wa dhabihu kuanzia mwanzo hadi mwisho.
Taasisi imerahisisha mchakato wa uchangiaji ili kuruhusu kila Muumini kupata fursa ya kuvuna thawabu maradufu. Kwa gharama ya TSH 130,000 kwa kila Qurbani, unaweza kukamilisha ibada yako kupitia njia zifuatazo:
- Mpesa: 0663582651
- Habib Bank (A/C No): 0000-639-0001
- Exim Bank (A/C No): 008-002-7061
- Jina la Akaunti: The Bilal Muslim Mission of Tanzania
Pia unaweza kuchangia kupitia akaunti ya world federation kupitia link ya donate.wf
