Office Hours
Mon-Fri: 08:30am-05:30pm Saturday: 08:30am-01:30pm

BMMT HQ Yaadhimisha Siku ya Wafanyakazi Duniani kwa Mechi ya Kirafiki na Wanafunzi wa Hawza ya Temeke

Picha ya pamoja ya wachezaji

DAR ES SALAAM, Mei Mosi 2026 – Katika kuadhimisha Siku ya Wafanyakazi Duniani (Mei Mosi), Makao Makuu ya Bilal Muslim Mission of Tanzania (BMMT HQ) wamesherehekea siku hii kwa namna ya kipekee kupitia mchezo wa kirafiki wa mpira wa miguu dhidi ya wanafunzi wa Hawza ya Bilal iliyopo Temeke.

Mechi hiyo ya kusisimua iliyochezwa katika viwanja vya Jakaya Kikwete Youth Academy (Mnazi Mmoja), jijini Dar es Salaam, ulikuwa ni zaidi ya mchezo wa uwanjani; ulikuwa ni ishara ya umoja, upendo, na kuimarisha mahusiano kati ya watendaji wa taasisi na vijana wanaolelewa kitaaluma na kidini.

Undugu na Ushirikiano Uwanjani

Mchezo huo uliwakutanisha wafanyakazi kutoka idara mbalimbali za Bilal na wanafunzi wa dini (Hawza), lengo likiwa ni kujenga mshikamano, kuboresha afya, na kuondoa ukuta wa kiofisi ili kuleta udugu wa Kiislamu. Dakika tisini za mchezo huo zilijawa na ufundi, nidhamu ya hali ya juu, na ushindani wa kiungwana (Fair Play), ambapo hadi filimbi ya mwisho, timu zote zilitoka sare ya kufungana goli 1-1.

Kauli za Wadau

Akizungumza kwa niaba ya wanafunzi wa Hawza, mmoja wa vijana hao alieleza furaha yake kwa kusema:

“Mchezo huu umekuwa ni chachu ya morali kwetu. Sio tu kwamba umetupa nafasi ya kuonyesha vipaji tulivyonavyo nje ya masomo ya darasani, bali umetufanya tujihisi kuwa sehemu moja na viongozi wetu. Tunatamani michezo kama hii iwe endelevu.”

Picha ya timu ya wanafunzi wa Hawza ya The Bilal Muslim Mission of Tanzania – Temeke.

Kwa upande wa uongozi na wafanyakazi wa Bilal Muslim Mission of Tanzania, alisisitiza kuwa michezo ni hitaji la msingi katika kuongeza ufanisi wa kazi.

“Tumetumia siku hii ya wafanyakazi kupata nishati mpya (recharging). Michezo inatusaidia kubadilishana mawazo na wanafunzi wetu katika mazingira rafiki, inajenga afya ya mwili na akili, na kutufanya turudi ofisini tukiwa na ari mpya ya kutoa huduma kwa jamii,” alisema Mussa Chamwene, Meneja Utawala.

Picha ya timu ya BMMT HQPicha ya timu ya wafanyakazi wa Taasisi ya The Bilal Muslim Mission of Tanzania (BMMT HQ) 

Tukio hili limeacha alama ya umoja ndani ya taasisi ya Bilal Muslim Mission of Tanzania, likionyesha kuwa katika kutoa huduma za kijamii na kidini, afya ya mtendaji na uhusiano wake na wale anaowahudumia ni nguzo muhimu. Sare ya goli moja kwa moja ni kielelezo tosha kuwa uwanjani sote ni washindi tunapocheza kwa ajili ya amani na mshikamano.

 

Imetolewa na:

Kitengo cha Habari na Mawasiliano,

The Bilal Muslim Mission of Tanzania.

About the Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

You may also like these

{title}