MAFUNZO YA IMAM HUSSEIN | HUSSEIN DAY 2023

 MAFUNZO YA IMAM HUSSEIN | HUSSEIN DAY 2023

Bilal Muslim Mission of Tanzania (BMMT) imeshiriki kwenye maonesho ya siku tatu ya Mafunzo ya Imam Hussein (a) ya mwaka 2023.

Maonesho hayo yalifanyika kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja, Dar Es Salaam kuanzia Septemba 14 hadi Septemba 16, 2023. Katika maonesho hayo maelefu ya watu kutoka maeneo mbalimbali ya jiji la Dar Es Salaam na maeneo ya jirani walihudhuria.

Mbali na kujifunza kuhusu Imam Hussein (a) na tukio la Karbala, wahudhuriaji walipata fursa ya kujifunza kuhusu kazi zinazofanywa na BMMT kwenye eneo la Tabligh, Elimu, Afya, Uchumi na Jamii kwa ujumla.

Mambo mengine yaliyofanyika ni, kambi ya afya na macho bure na zoezi la uchangiaji damu kwa muda wa siku tatu mfululizo, huku maoeneosho hayo yakifugwa kwa majlis maalumu iliyofanyika usiku wa siku ya tatu.

Maonesho hayo hufanyika mara moja kila mwaka, huandaliwa na Khoja Shia Itha-Asheri Jamaat ya Dar Es Salaam (KSIJ Dar Es Salaam) kwa kushirikiana na Bilal Muslim Mission of Tanzania na taasisi nyingine za kishia kutoka ndani na nje ya nchi.

MATUKIO KATIKA PICHA:

Newsletter: Swahili version

Please wait while flipbook is loading. For more related info, FAQs and issues please refer to DearFlip WordPress Flipbook Plugin Help documentation.

Newsletter: English version

Please wait while flipbook is loading. For more related info, FAQs and issues please refer to DearFlip WordPress Flipbook Plugin Help documentation.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *