151 WAHITIMU PROGRAMU YA MASOMO YA KIISLAMU KWA NJIA YA POSTA & MTANDAO

Wanafunzi 151 wamehitimu Kozi ya Masomo ya Kiislamu kwa Njia ya Posta & Mtandao mwaka 2023.

Sherehe za Mahafali zilifanyika Husseynia – Bilal, Temeke tarehe 4 Novemba 2023 huku Sheikh Ramadhan Kwezi akiwa mgeni rasmi.

Hafla hiyo ilipambwa na uwepo wa Sheikh Msabaha Mapinda – Mkuu wa Tableegh BMMT, Masheikh kutoka Hauzat Bilal Temeke, na wahitimu wenyewe.

Sehemu ya shughuli zilizofanyika ni, kisomo cha Quran, Hadithul kisaa, Mawaidha, Zoezi la kutunuku vyeti, na kupata chakula cha mchana cha pamoja baada ya swala ya Jamaa.

           

Katika mwaka wa 2023, jumla ya wanafunzi 211 walijiunga na Masomo ya Msingi ya Kiislamu, wanafunzi 132 sawa na 63% walihitimu. Pia tulifanikiwa kufufua Kozi ya Masomo ya Juu ya Kiislamu katika mwaka huu (2023), wanafunzi 26 waliandikishwa. Wanafunzi 19 sawa na 76% walihitimu.

Tunatoa shukrani zetu kwa Bilal Muslim Mission of Tanzania na Africa Federation kwa udhamini wa programu hii. Pia tunaishukuru Bilal Comprehensive School (BCS) na Hawzatu Bilal Temeke kwa mchango wao uliowezesha kufanikisha tukio hili.

About the Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

You may also like these