Kuhusu Programu:
Karibu kwenye Programu ya Masomo ya Kiislamu kwa njia ya Posta na Mtandao “MASOMO YA JUU YA KIISLAMU”. Programu hii inahusisha vitabu vine (Kitabu cha kwanza, Kitabu cha pili, Kitabu cha tatu & Kitabu cha nne).
Mfumo wa Masomo:
Kuna njia mbili za kushiriki kwenye program hii.
(1) Masomo ya Kiislamu kwa njia ya Posta
Kama upo Dar es salaam, fika Makao Makuu ya Bilal Muslim Mission of Tanzania (BMMT), Mtaa wa Libya karibu na kituo cha mwendokasi Kisutu. Kujaza fomu ya Usajili, kisha utapatiwa vitabu na maelezo mengine.
Kama upo nje ya Dar es Salaam (Tanzania) na huwezi kufika ofisini, wasiliana na mratibu wa programu kupitia baruapepe: bookshop@bilal.or.tz au namba ya simu +255 678 888 795 upate maelekezo ya kupata fomu ya usajili, vitabu na namna ya kutuma mitihani na maelezo mengine.
(2) Masomo ya Kiislamu kwa njia ya Mtandao
Kama upo nje ya Tanzania au upo Tanzania lakini ungependa kusoma kupitia mtandao, tembelee tovuti ya taasisi www.bilal.or.tz kupata Fomu ya usajili pamoja na Vitabu.
Baada ya kujaza fomu ya usajili, itume kwa mratibu wa programu kupitia baruapepe: bookshop@bilal.or.tz au namba ya simu +255 678 888 795 (Whatsapp) upate maelekezo mengine yakiwemo, namna ya kutuma mitihani.
ZINGATIA: KWA MWANAFUNZI WA MASOMO YA JUU YA KIISLAMU, HAKIKISHA UNAAMBATANISHA NAKALA YA CHETI CHA MASOMO YA MSINGI YA KIISLAMU (PDF)
Bofya hapa kupakua Fomu ya usajili
Mtume Muhammad (s) amesema, “Kutafuta elimu ni wajibu kwa kila Muislamu Mwanaume na Mwanamke”.