BMMT YAKAMILISHA MAREKEBISHO MAKUBWA YA MIUNDOMBINU YA KITUO CHA KILWA.

 BMMT YAKAMILISHA MAREKEBISHO MAKUBWA YA MIUNDOMBINU YA KITUO CHA KILWA.

Bilal Muslim Mission of Tanzania (BMMT) inayoyofuraha kutoa taarifa za kukamilika kwa ukarabati wa miundombinu katika kituo cha BMMT Kilwa kilichopo Wilaya ya Kilwa mkoani Lindi. Ukarabati huu mkubwa ulianza Oktoba, 2022 na kukamilika Mei 2023. Mindombinu iliyorekebishwa ni pamoja na jengo la msikiti, nyumba ya mwalimu, jengo la madrasa pamoja na ujenzi wa vyoo vipya. Ukarabati pia ulihusisha uboreshaji wa miundombinu ya maji na umeme kwenye majengo yote, pamoja na kupaka rangi ndani na nje ya majengo hayo.

Kituo cha Kilwa ni miongoni mwa vituo vikongwe kilichoanzishwa na Jumuiya za kikhoja huko kusini mwa Tanzania.

Katika miaka ya 1960 na 1980 baadhi ya vituo vilivyoanzishwa na Jumuiya ya kikhoja havikuwa vikitumika hivyo, vilikabidhiwa kwa ajili ya kuendeshwa na kuendelezwa na Bilal Muslim Mission of Tanzania. Vituo hivyo ni Nachingwea, Mtama, Tunduru, Bagamoyo, Tabora, Kasulu, na Mingoyo. Vituo vya Lindi, Singea na Mikindani bado vinajamii za kikhoja.

Kulingana na Afrika Federation, Jamii za kikhoja zilianza kuingia Kilwa kuanzia mwishoni mwa miaka ya 1800 wakijihusisha na biashara mbalimbali zikiwemo za maduka. Inaelezwa kwamba, katika mwaka 1906 baada ya kutuma maombi, utawala wa kijerumani katika wilaya ya Kilwa uliwapatia ardhi (kiwanja) katika kiwanja hicho palijengwa msikiti, ukumbi, (husaynia) na madrasa, ambavyo vipo hadi sasa. Mradi huu unatajwa kukamilika mnamo mwaka 1912.

Mradi huu ulifadhiliwa na wafadhili mbalimbali kupitia Africa Federation. Aidha, Bilal ilipokea fedha kutoka kwa wafadhili wengine binafsi, fedha hizo zilitumika kukarabatimajengo ya msikiti katika kituo cha Mtama na Mingoyo huku msikiti wa Nachingwea ukibomolewa na kujengwa upya.

PICHA KABLA YA UKARABATI

                             

PICHA WAKATI WA UKARABATI

                              

PICHA BAADA YA UKARABATI

                              

Tunawakaribisha wafadhili wote na wale wenye kuitakia mema BMMT kufadhili marekebisho ya jengo la msikiti wa Bagamoyo. Eneo la paa katika jingo hilo linahitaji maboresho kutokana na uharibifu wa muda mrefu.

BMMT inapenda kutoa shukrani za dhati kwa AFED na kwa wafadhili kuitokana na msaada wao unapelekea mafaniio haya. Mwenyezi Mungu atawalipa Zaidi.

###

Imetolewa na:

Idara ya Habari & Mahusiano.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *