Taasisi ya Bilal Muslim Mission of Tanzania (BMMT) inakutangazia fursa ya kujiunga na Masomo ya Kiislamu yanayotolewa kwa njia ya Posta au Mtandaoni (Online).
Fursa hii ipo wazi muda wote, kwa watu wa kada zote kutoka popote ulimwenguni. Malengo ya masomo haya ni kuwaongezea watu maarifa kuhusu dini ya Kiislamu.
Kwa maelezo zaidi na namna ya kijiandikisha, fika ofisi kuu za Bilal zilizopo Mtaa wa Libya karibu na kituo cha mwendokasi Kisutu au wasiliana nasi kupitia nambari za simu: +255 678 888 795 au barua pepe: bookshop@bilal.or.tz