UJUMBE WA MAINSTAY FOUNDATION (TMF) WAKUTANA NA WANUFAIKA WA MRADI WA TMF EDUCATION SUPPORT SCHEME.

Tarehe 1 Juni, 2024, ujumbe kutoka Taasisi ya The Mainstay Foundation-UK (TMF-UK), ukiongozwa na Mdhamini na Mwanzilishi wa TMF, Syed Hassan al- Hakim aliyeambatana na Alhaj
Yasser Bashar, ulikutana na wanufaika wa TMF Education Support Scheme jijini Dar es  Salaam. Mkutano huo ulifanyika katika Kituo cha Mafunzo chaAfrica Federation (AFED) na kusimamiwa na Bilal Muslim Mission of Tanzania (BMMT).

Hafla hiyo ilihudhuriwa na wajumbe kadhaa wa bodi ya BMMT, akiwemo Mwenyekiti Alhaj Hussein Karim, Makamu Mwenyekiti Alhaj Abdul-Wahid Mohammed, Mtendaji Mkuu Nd. Hafidhi Mansour, Mkuu wa Tabligh Sheikh Msabaha Mapinda , Mwenyekiti wa BMMT Kanda ya Pwani na Kusini Alhaj AzizHussein Rajani, Meneja Miradi Dada Nasra Salehe, wanufaika – wanafunzi wa shahada ya kwanza, na wageni wengine waalikwa.

Hafla hilo lilianza kwa usomaji wa Qur’an na Nd. Ali- Haidary Abdul-Wahid Mohammed, akifuatiwa na hotuba ya ufunguzi kutoka kwa Alhaj Hussein Karim. Katika hotuba yake, Alhaj Hussein Karim alitambulisha ujumbe wa The Mainstay Foundation kwa walengwa na kueleza madhumuni ya tukio hilo.

Wanafunzi hao walipata fursa ya kujitambulisha na kueleza kwa ufupi juu ya mchango wanaoupata kupitia mradi wa Mpango wa Kusaidia Elimu wa TMF katika safari zao za kielimu, pamoja na changamoto mbalimbali zinazowakabili.

Katika hotuba yake, Syed Hassan al Hakim alitoa shukrani zake kwa BMMT kwa kuandaa hafla hiyo. Pia aliwashukuru wanafunzi kwa kupanga upya ratiba zao za mwisho wa wiki ili kuhudhuria
hafla hiyo. Alieleza TMF hufanya programu mbalimbali kwa kushirikiana na BMMT na mashirika mengine duniani kote, lengo likiwa ni kusaidia jamii za kishia, kama vile za Tanzania, ziweze
kuimarika katika sekta ya elimu na uchumi. Alisisitiza kuwa juhudi hizi zinalenga hatimaye kuboresha jamii ya kishia duniani kote.

Kufuatia hotuba yake, Alhaj Abdul-Wahid Mohammed alitoa shukurani zake na kusisitiza kuwa pamoja na mafanikio ya kiuchumi na kielimu, jamii za kishia zinapaswa pia kujitahidi kuboresha
akhlaq (tabia njema) zao ambazo zinakosekana katika jamii nyingi. Hotuba ya Alhaj Abdul-Wahid ilifuatiwa na kisomo cha Dua Al’Hujjah kilichoongozwa na Sheikh Msabaha Mapinda. Msimamizi wa Sherehe, Br. Hafidhi Mansour, alihakikisha tukio linaendelea vizuri na kwa kuzingatia muda.

TMF Education Support Scheme, mradi unaofadhiliwa na TMF na kutekelezwa kwa ushirikiano na BMMT, unafadhili vijana wa kishia katika ngazi mbalimbali za elimu—elimu ya ufundi, cheti,
stashahada na shahada ya kwanza—kwa kutoa mikopo ya masomo ili kutimiza ndoto zao za kielimu. Mradi huu ulianza kwenye mwaka wa masomo 2022/2023 na hadi kufikia mwisho wa mwaka wa masomo 2023/2024 jumla ya wanafunzi 307 walikuwa wamenufaika.

Kwa mara nyingine, BMMT iliishukuru TMF kwa kuendelea kushirikiana katika mradi huu na miradi mingineyo. Pia imetoa wito kwa wanufaika wote kuwekeza nguvu zao katika kutimiza
malengo ya mradi na kurejesha mikopo hiyo kwa uaminifu ili fedha hizo zitumike kusaidia wahitaji wengine.

About the Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

You may also like these