UONGOZI WA BMMT KANDA YA PWANI & KUSINI WAFANIKIWA KUENDESHA SEMINA YA MWAKA 2023

Picha kutoka kushoto kuelekea kulia: Msimamizi wa Tabligh Kanda ya Pwani na Kusini – Sheikh Swahib Rashid, Mtendaji Mkuu BMMT – Ndugu Hafidhi Mansour, Makamo Mwenyekiti BMMT – Haj Abdul-Wahid Mohammed, Mkuu wa Tabligh BMMT – Samahat Sheikh Msabaha Mapinda. | Picha na: Rajabu Ngwame.

Bilal Muslim Mission of Tanzania (BMMT) kupitia uongozi wake wa Kanda ya Pwani na Kusini umefanikiwa kuendesha Semina ya kila mwaka kuanzia Jumatatu tarehe 18 hadi Jumapili tarehe 24 Disemba 2023.

Semina hiyo imefanyika Hauzatu Bilal Temeke na ilihudhuriwa na zaidi ya washiriki 38 kutoka mikoa ya Dar es Salaam, Pwani, Lindi, Mtwara, Ruvuma, and Morogoro.

Semina ilifunguliwa rasmi kwa hotuba ya Haj Abdul-Wahid Mohammed, Makamo Mwenyekiti BMMT, na ilifungwa kwa hotuba ya Haj Hussein Karim, Mwenyekiti BMMT.

Semina ilipata heshima ya kuwa na wazungumzaji wakiwemo; Ndugu Hafidhi Mansour – Mtendaji Mkuu BMMT, Msimamizi wa Tabligh Kanda ya Pwani na Kusini – Sheikh Swahib Rashid, Afisa Utawala Kanda ya Pwani na Kusini – Ndugu Sinani Kamegi, Mkuu wa Iadara ya Habari & Mahusiano BMMT – Ndugu Rajabu Ngwame.

Wengine ni; Alhaj Haji Sahib Rajani, Dkt. Mohsen Maarefi, Sheikh Abdul Rahman, Dkt. Shabir Khalfan, Sayyid Mansour Musawy, Sheikh Ramadhan Kwezi, Sheikh Thukmal Hussein, Ndugu Aziz Sharif and Ndugu Burhan Haroun.

Mada mbalimbali juu ya Andalio & Tathmini ya Somo, Uongozi & Maadili, Maendeleo ya Jamii, Mahusiano ya Umma, Mirathi, na Ajenda mbalimbali katika ulimwengu wa Kiislamu zilijadiliwa.

Baadhi ya watumishi walitambuliwa na kupatiwa zawadi kutokana na utumishi wao uliotukuka katika kipindi cha mwaka 2023.

Katika siku ya mwisho ya semina, washiriki wote walipatiwa vyeti vya ushiriki na walipata fursa ya kufanya ziara kwenye viwanja vya Kabristani na kusoma dua kwa ajili ya Marhoum Allamah Sayyid Saeed Akhtar Rizvi – mmoja wa waasisi wa BMMT pamoja na Marhoumeen wengine walioshiriki katika kuiunda na kuiendeleza taasisi.

                                                                                                                                                                    

Sekretariet ya BMMT inatanguliza shukrani za dhati kwa Uongozi wa BMMT, Africa Federation (AFED), kamati tendaji na watu wote waliojitolea kufanikisha semina hii.

Tunawaombea baraka na umri mrefu wote waliotoa mchango wao wa hali na mali uliopeleka mafanikio ya semina kwa mwaka 2023. Mwenyezi Mungu awafungulie zaidi katika shuguli zao, Ameen.

###

Imetolewa na:

Idara ya Habari & Mahusiano

BMMT – Makao Makuu, Dar es Salaam,

About the Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

You may also like these