ZIARA YA KAIMU SHEIKH MKUU WA DAR ES SALAAM BMMT

Kutoka kushoto kuelekea kulia: Sheikh Walid Alhadi – Kaimu Sheikh wa Mkoa wa Dar Es Salaam, Sheikh Msabaha Mapinda – Mkuu wa Tabligh BMMT Taifa.

Sheikh Walid Alhadi – Kaimu Sheikh Mkuu wa Dar Es Salaam ameipongeza Bilal Muslim Mission of Tanzania (BMMT) kwa kazi kubwa inayoifanya hususani kwenye nyanja ya elimu.

Sheikh Walid ametoa pongezi hizo, Novemba 8, 2023 alipofanya ziara katika shule ya Bilal Comprehsive na Hauza ya Bilal Temeke.

Amesema, ameridhika kwa kile alichokiona katika kazi ambazo zinafanywa na BMMT na kuwatia moyo waalimu na viongozi kuendeleza utekelezaji wa majukumu yao ya kila siku kwa ajili ya Mwenyezi Mungu.

Aidha, Sheikh Walid amesema, ameitumia ziara hii kujitambulisha kwetu na kufungua mlango wa mashirikiano baina ya ofisi yake na taasisi yetu.

bofya hapa Kutazama alichokisema Sheikh Walid Alhadi

Katika ziara hii, Sheikh Walid aliambatana na ujumbe wake ukiongozwa na Sheikh Zairai Mkoyogole – Sheikh Mkuu wa wilaya ya Temeke.

BMMT kwa upande wake iliwakilishwa na Ndugu Hafidhi Mansour – Mtendaji mkuu aliyeambatana na Sheikh Msabaha Mapinda – Mkuu wa Idara ya Tabligh.

Wengine waliokuwepo ni Uongozi wa Hauzatu Bilal Temeke ukiongozwa na Sheikh Muhammad Yusuph – Mdiru wa Hauzatu Bilal, na Mama Siddika Karim – Mkuu wa shule ya Bilal pamoja na timu yake.

BMMT imefurahishwa na ziara hiyo na inaahidi kuendeleza ushirikiano mwema na taasisi nyingine yoyote kwa ajili ya Mwenyezi Mungu.

MATUKIO KATIKA PICHA | ZIARA YA KAIMU SHEIKH MKUU WA DAR ES SALAAM BMMT

About the Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

You may also like these