BMMT YAZINDUA MSIKITI WA ZAINUL ABIDEEN (A.S) UVINZA, KIGOMA.

Bilal Muslim Mission of Tanzania (BMMT) inayofuraha kuwajulisha kwamba, imezindua msikiti mpya uliopewa jina la Imamu wetu wa nne, Imam Ali Zainul Abedeen (A.S) huko Uvinza Kigoma – magharibi mwa Tanzania.

Sherehe za uzinduzi wa msikiti huo zilifanyika Juni 30, 2024 na kupambwa na uwepo wa Sheikh Hashimu Kapipi akimuwakilisha Sheikh Mkuu BAKWATA mkoa wa Kigoma, Sheikh Hassan Kiburwa. Sherehe hiyo pia ilihudhuriwa na Haj Hussein Karim – Mwenyekiti BMMT na Haj Hafidhi Mansour – Mtendaji mkuu BMMT.

Mlezi wa kituo cha BMMT Uvinza Haj Maqbul Jaffer alisimamia zoezi la kukusanya fedha kutoka kwenye familia yake, marafiki na wafadhili mbalimbali na kufanikisha ujenzi wa msikiti huo.

UVINZA INAPATIKANA WAPI?

Uvinza ni moja ya tawala za wilaya za mkoa wa Kigoma nchini Tanzania. Mji wa Uvinza upo mashariki, umbali wa takribani kilimota 100 kutoka makao makuu ya mkoa Kigoma. Eneo hilo linafahamika zaidi kihistoria kwa uzalishaji wake wa chumvi nchini Tanzania.

MATUKIO KATIKA PICHA:

         

BMMT inapenda kuwashukuru wafadhili wote pamoja na Alhaj Maqbul na familia yake kwa kujitolea kwao katika mradi huu pamoja na usimamizi wa shughuli za Bilal Uvinza. Tunamuombea kwa Mwenyezi Mungu (S.W.T) ampe maisha marefu yenye afya tele, fanaka na tawfiq katika utumishi wake pamoja na marehemu wake wote.

About the Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

You may also like these