Bilal Muslim Mission of Tanzania (BMMT) imegawa zaidi ya tablets 100 kwa wanafunzi wake wa Hauzat Ahlul-Bayt (Wavulana), Hauzat Sayyida Maasoumah (Wasichana) za Dar es Salaam na Hauzat Qaim (Wavulana) ya Tanga, jambo ambalo linatarajiwa kurahisisha na kuongeza kasi ya mchakato wa kujifunza.
Katika mradi huu wa majaribio tablet zilitolewa kwa wanafunzi wa madarasa ya juu pekee.
Mradi huu umefadhiliwa na The World Federation of Khoja Shia Ithana-Asheri Muslim Communities. Katika hatua hii ya majaribio, mradi huo umetekelezwa katika hauza tatu tu. Aidha, wanafunzi wanaoendelea na masomo ya juu nje ya nchi pia walipatiwa tablet hizo ili kuwasaidia kwenye masomo yao.
Tablet zote, ziliwekwa vitabu vyote muhimu sambamba na program zinazohusiana na masomo ya dini. Wanafunzi wa hauza pia wanafundishwa masomo kadhaa yanayohusiana na matumizi ya tablet na computer kama vile; Ms. Word, Excel, Baruapepe na mtandao (Internet) na namna ya kutumia mitandao ya kijamii kwa shughuli za kitabligh.
Katika mwaka huu, wanafunzi nane kati ya 12 waliohitimu wamejiunga katika chuo cha Alawiya, Najaf kwa ajili ya kuendelea na masomo ya juu ya Fiqh, Aqida, Lugha ya Kiarabu n.k. Wanafunzi wote walipatiwa tablet ili kuwasaidia kwenye masomo yao.
Tunapenda kuishukuru Idara ya Mambo ya nje ya Tabligh ya The World Federation kwa kugharamia nauli za safari pamoja na viza za wanafunzi hao wote.
MATUKIO KATIKA PICHA:
Kwa mara nyingine, BMMT inapenda kuwashukuru wafadhili wa mradi kwa msaada wao uliowezesha utekelezaji wa mradi huu wa majaribio. Pia, inakaribisha wafadhili wengine na watu wenye mapenzi mema na taasisi yetu kutuunga mkono katika kuzifikia hauzat nyingine za Tanga, Kigoma, Morogoro (Rudewa), Kagera (Bukoba), Kilimanjaro (Moshi) na Ruvuma (Songea).