UFUNGUZI WA MZEE HASSANALI NA MAMA FATEMABAI DEWJI ISLAMIC CENTRE.

Bilal Muslim Mission of Tanzania (BMMT) ilizindua Kituo cha Kiislamu cha Mzee Hassanali na Mama Fatemabai Dewji kilichopo Mabibo Dar-es-Salaam, kituo kilichotolewa na Familia ya Alhaj
Gulam Dewji kutumika kama Hauzatu Sayyida Maasoumah .

Hafla hiyo ilifanyika Jumamosi Juni 22, 2024 na ilipambwa na uwepo wa ujumbe wa Familia ya Dewji ukiongozwa na Alhaj Gulam Dewji ambaye alikuwa Mgeni Rasmi na mjukuu wake Abbas
Mohammed Dewji mbele ya wajumbe wa Ofisi ya AFED wakiongozwa na Mwenyekiti wake Alhaj Amine Nassor. Wengine waliohudhuria ni Mdhamini na Mwenyekiti wa Awali wa AFED Alhaj
Shabir Najafi na Makamu wa Rais wa Khoja Shia Ithna-Asheri Jamaat ya Dar es Salaam Alhaj Abdulrasul Shamji.

Kutoka BMMT hafla hiyo ilihudhuriwa na Mwenyekiti Alhaj Hussein Karim, Mtendaji Mkuu Bw. Hafidhi Mansour, Mkuu wa Tableegh Sheikh Msabaha Mapinda pamoja na wafanyakazi
wengine wa Makao Makuu. Walimu, wafanyakazi na wanafunzi kutoka Hauzatu Sayyida Maasoumah na Hauzatu Bilal pia walihudhuria.

Baada ya kukata utepe, wageni waalikwa walipata fursa ya kutembelea na kukagua mradi huo. Ukarabati wa mradi huo ambao ulichukua zaidi ya miezi sita ulilenga kuweka jiko la kisasa, eneo
la msikiti, maktaba, chumba cha kompyuta, madarasa, ofisi za waalimu, ukumbi wa kulia chakula, vyumba vya kulala, miundombinu ya maji taka na usafi wa mazingira n.k.

Hafla hiyo pia ilisherehekea mahafali ya wanafunzi 12 kutoka Hauzatu Bilal (Wavulana), huku wanafunzi wanane wakitarajia kuendelea kimasomo nchini Iraq. Mafanikio yao
yalitambuliwa kwa tuzo za ubora wa kitaaluma na nidhamu ya kuigwa.

 

Hafla hiyo ilianza kwa kisomo cha Qur’ani Tukufu na Sheikh Al Amin wa Hauzatu Sayyida Maasoumah, na kufuatiwa na Hadith ul Kisaa na Nasru Haji Mnyonge wa Hauzatu
Bilal. Bw. Hafidhi Mansour alifanya muhtasari toa muhtasari wa shughuli za Hauzatu Sayyida Maasoumah.

           

Katika hotuba yake, Mwenyekiti wa BMM T Alhaj Hussein Karim alimshukuru Alhaj Gulam Dewji kwa kutoa msaada sio tu wa kituo hicho bali pia kufadhili ukarabati wake na msaada wake
endelevu. Aidha, alitoa shukurani kwa mwenyekiti wa AFED Alhaj Amine Nassor na mtangulizi wake Alhaj Shabir Najafi kwa upande wao katika makabidhiano mazuri ya mradi huo kutoka
AFED hadi BMMT.

Alifahamisha kuwa, mradi huu umetolewa kwa Hauza ya wasichana kwa kutambua wajibu wao kama walezi wa jamii. Hivyo, wanahitaji maarifa ya kutosha ya kiroho na kijamii ili
kushughulikia vyema jukumu lao. Aliwapongeza wanafunzi wa mwaka wa nne wa shule ya Hauzatu Bilal kwa kumaliza masomo yao na kuwataka waliopata fursa ya kwenda Iraq kwa masomo zaidi wawe mabalozi bora wa Bilal na Tanzania kwa ujumla.

Akizungumza kwa niaba ya familia ya Dewji , Alhaj Zulfikar Chandoo alitoa pongezi kwa kutambua kazi ya kupongezwa ya kueneza neno la Mwenyezi Mungu (SWT) na mafundisho ya Mtume Muhammad ( saww ) na kizazi chake ( as ) inayofanywa na AFED na BMMT na kumuomba Mwenyezi Mungu azitambue juhudi zao na kuwalipa kwa wingi. Pia alimshukuru Mwenyezi Mungu (SWT) kwa baraka na fursa ya kuwa sehemu ya kazi tukufu kwa kuungana na BMMT iliyofanikisha kufunguliwa kwa Kituo cha Kiislamu cha Mzee Hassanali na Mama Fatemabai Dewji. Aliongeza, ni jambo la kuridhisha kuona kituo hicho kitawawezesha dada zetu kufikia matarajio yao katika mazingira salama. Alimalizia kwa kusema kuwa, familia kupitia taasisi ya Mo Dewji Foundation imekuwa ikitoa chachu cha matokeo endelevu nchini Tanzania katika nyanja ya elimu, utoaji wa huduma za afya na upatikanaji wa maji safi na salama kwa jamii zisizo na uwezo. Alikaribisha
muungano wa BMMT na Mo Dewji Foundation katika kuinua jumuiya za Kiislamu kwa radhi za Allah (SWT).

Mdhamini na Mwenyekiti wa Awali wa AFED Alhaj Shabir Najafi alizungumzia kuridhishwa kwake na mabadiliko ya haraka ya jengo hilo na kueleza furaha yake kuona viwango vya juu
vilivyowekwa kwa jengo hilo. Alimpongeza Alhaj Hussein Karim na kumshukuru Alhaj Gulam Dewji kwa kazi nzuri na kuihakikishia Bilal kuwa ataendelea kuiunga mkono katika harakati zake.

Alhaj Amine Nassor, Mwenyekiti wa AFED, alisifu kituo hicho na kusisitiza umuhimu wa maendeleo ya kiroho katika Hauzatu Sayyida Maasoumah . Alimpongeza Alhaj Gulam Dewji kwa ukarimu na kujitolea kwake katika kusaidia mipango ya kielimu, kwa kuakisi misingi ya Sayyida Khadijatul Kubra (a.s). Alhaj Amine Nassor pia alimpongeza Alhaj Hussein Karim kwa hatua iliyofikiwa katika Hauza hiyo ya wavulana wanane na wasichana kumi wakijiandaa kwenda nje ya nchi kwa masomo zaidi wanapohitimu mwaka huu.

Bw. Nasru Mnyonge , mwakilishi wa wanafunzi waliohitimu, aliwahimiza wanafunzi wenzake kuendelea kuwa imara katika safari yao ya elimu. Aliwashukuru walimu na menejimenti ya BMMT
kwa msaada wao thabiti, na kuahidi kuzingatia maadili waliyopandikizwa wanapoendelea na masomo zaidi nje ya nchi.

Sheikh Msabaha Mapinda alitoa hotuba ya kuhitimisha, akisisitiza umuhimu wa kituo hicho kipya kukuza ubora wa elimu na ukuaji wa kiroho miongoni mwa wanafunzi wake. Alisisitiza kwa wale wanaojiandaa kusafiri nje ya nchi kwa ajili ya masomo zaidi kuwa mabalozi wazuri wa BMMT na Tanzania kwa ujumla. Hafla ilihitimishwa kwa dua ya kuomba baraka na ustawi wa Hauzatu Sayyida Maasoumah ikioongozwa na Sheikh Msabaha .

MC wa programu, Sheikh Swahib Rashid aliendesha hafla hiyo vizuri sana na alikuwa makini katika kuchunga wakati kulingana na utaratibu wa programu.

MATUKIO KATIKA PICHA:

About the Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

You may also like these