BMMT KWENYE MAADHIMISHO YA MAULID YA MTUME MUHAMMAD (S.A.W.W) – 2023

Kutoka kushoto kuelekea kulia: Ndugu Athumani Kagimbo, Sheikh Msabaha Mapinda, Dkt. Khatib, Sayyid Aidarus Alawy, Haj Hussein Karim, Sheikh (Dkt) Abdulrazak Amir, Haj Aunali Khalfan, Haj Abdulwahid Mohammed | Picha na Yusuph Sambiga

Waislamu duniani kote wanaadhimisha kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Mtukufu Mtume Muhammad (s.a.w.w) ambaye alizaliwa Makkah mwaka wa 570 mwaka wa tembo na kuwa mtu aliyeheshimika, aliyejulikana kwa uadilifu na uaminifu. Akiwa na umri wa miaka 40, alipata wahyi wake wa kwanza (ufunuo kutoka kwa Allah S.W.T). Safari yake kama mjumbe wa mwisho wa Allah S.W.T ilianza.

Bilal Muslim Mission of Tanzania (BMMT) ilifanya hafla kubwa ya Maulid Unity Hall, Dar Es Salaam mnamo tarehe 29 Oktoba 2023. Zaidi ya watu 2000 kutoka Dar Es Salaam na maeneo ya jirani walihudhuria.

Hafla hiyo ilipambwa na mahudhurio ya Haj Aunali Khalfan – Makamu mwenyekiti wa Africa Federation (AFED), Haj Hussein Karim – Mwenyekiti BMMT, Haj AbdulWahid Mohammed – Makamu mwenyekiti BMMT, Sheikh Msabaha Mapinda – Mkuu wa Tabligh BMMT, Hafidhi Mansour – Mtendaji mkuu BMMT na wageni wengine waalikwa ikiwa ni pamoja na madrasa kadhaa za kisunni.

                                   

Wazungumzaji wakuu, Sheikh (Dr.) Abdul-Razak Amir na Sayyid Aidarus Alawy walipata fursa ya kuzungumza huku wakiakisi kaulimbiu ya mwaka huu ya “Uislamu na Maadili”

                   

Maulid kwenye baadhi ya vituo vya BMMT

Vituo vyote vya Bilal vilifanya sherehe za Maulid katika vijiji vyao, baadhi vilikuwa na mfululizo wa majalis (Wiki ya Muhammad). Madrasa za kisunni jirani na vituo hivyo pia zilialikwa.

           

Ujumbe juu ya Uislamu na Maadili ulivuma kwenye vituo vyote.

Bilal Muslim Mission of Tanzania inatanguliza shukrani kwa wafadhili kutokana na michango yao iliyosaidia kufanikiwa kwa uendeshaji wa programu za Maulid.

Bilal Muslim Mission of Tanzania | S.L.P 20033, Dar Es Salaam | Simu: +255 745 111 150 |Barua pepe: admin.bilaltz@africafederation.org | Tovuti: www.bilal.or.tz

Imetayarishwa na:

Idara ya Habari & Mahusiano

Novemba, 2023.

About the Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

You may also like these