KITABU | HUKUMU ZA IBADA KWA UFUPI | KWA MUJIBU WA FAT’WA ZA AYATULLAH SAYYID ALI HUSEINI SISTANI (Mwenyezi Mungu amjaalie umri mrefu)

 KITABU | HUKUMU ZA IBADA KWA UFUPI | KWA MUJIBU WA FAT’WA ZA AYATULLAH SAYYID ALI HUSEINI SISTANI (Mwenyezi Mungu amjaalie umri mrefu)

UTANGULIZI WA MCHAPISHAJI

Sifa zote njema zinamstahiki Mwenyezi Mungu Mwingi wa Rehema Mwenye Kurehemu, Muumba na Mlezi wa viumbe vyote. Kisha Swala na Salamu zimuendee Mtukufu wa Daraja Mtume wetu Muhammad (S.A.W.W) pamoja na kizazi chake kitukufu.

Ndugu msomaji, kitabu hiki ni mukhtasari wa baadhi ya Mas’ala yanayohusu hukumu za sharia na kimekusanya mambo muhimu ya ibada ya swala na mengineyo yanayohitajika kufanywa kabla ya swala kama vile tohara na kadhalika.

Hukumu nyingine zilizokusanywa kwenye kitabu hiki ni pamoja na: hukumu za swaumu, hija, zaka, khumsi, na pia umo muhtasari wa mafunzo yanayohusu hukumu za taqlid, kuamrisha mema na kukataza maovu.

Mas’ala yote yaliyomo ndani ya kitabu hiki ni kwa mujibu wa fat’wa za Ayatullah Al-Udhma Sayyid Ali Husaini Sistani.

###

Changia gharama za uchapishaji kwa kununua kitabu hiki kwa Tsh 2,000/= dukani kwetu au pakua kitabu hiki (bure) hapa kwa matumizi binafsi ya kusoma na kujifunza.

Please wait while flipbook is loading. For more related info, FAQs and issues please refer to DearFlip WordPress Flipbook Plugin Help documentation.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *